Hikaya za Anatolia

Hikaya za Anatolia

Hikaya za Anatolia

Leo katika hikaya za Anatolia tunakuleteeni hikaya ya mungu kati ya miungu w azama hizo aliyekuwa akijulikana kwa jina la Zeus .Siku moja Zeus alikuwa amekaa chini ya mti wa mhadasi na kumuona msichana mmoja mzuri sana.Zeus kumuona huyo msichana akampenda .Msichana huyo alikuwa nim toto wa mfalme .Zeus katika muda mfupi aliweza kumwambia binti yule jinsi anavyompenda na hatimaye binti akakubali upendo wake.Basi walikuwa wakipendana sana kiasi kwamba hawakuweza kukaa hata sekunde moja bila kuonana.Walikuwa wakikutana chini ya mti ule kila mara.Mke wa kwanza wa Zeus akaja kufahamu kuwa mume wake anamdanganya na anapendana na msichana mwingine.

Basi mwanamke huyo alivumilia kwa muda mrefu lakini mwishowe uzalendo ukamshinda.Akapuliza wingu moja ambalo linempata binti yule na kumpeperusha mpaka mwisho wa mbingu ambapo asingeweza kurudi tena.Zeus alipojua hilo aliamua kumbadilisha msichana yule kuwa ndama nyeupe.Aliamini kuwa hio ndio ilikuwa njia pekee ya kumuokoa binti yule.Mke wa Zeus akataka mume wake amletee ndama nyeupe.Kwa shingo upande Zeus akampelekea mke wake ndama huyo.Mke wake akamuita Argos na kumpa ndama huyo kwa sharti kwamba asikubali ndama huyo aende mahala popote.Argos akaichukua ndama hiyo na kuifungiamchana na usiku asiiruhusu kwenda mahala popote.

Zeus alikuwa akisikitishwa sana na matendo hayona hivyo siku moja akamuita mtoto wake Hermes na kumtaka amchukue ndama huyo kutoka kwa Argos aliyekuwa na jicho la usoni.Basi Hermes akampigia filimbi Argos na kumfanya alale.Wakati akiwa usingizini Hermes alimtegeshea tu pale atakapolala amuue.Argos alipofumba jicho tu Hermes aliweza kummaliza hapohapo.Akamchukua ndama yule na kumpeleka na kumpa pange awe anamsindikiza kila aendapo.Basi msichana huyo alikuwa akitembea Istanbul nzima akiwa anasindikizwa na pande hiyo na ndo maana daraja la Bhosphorus lina jina hilo likiamini kuwa ndama huyo alipita pale usiku mmoja.

Tukutane tena katika hikaya nyingine motomoto za Anatolia.Habari Zinazohusiana