Uturuki yatoa fursa ya udhamini wa masomo

Uturuki yatoa fursa ya udhamini wa masomo kwa wanafunzi kutoka katika pembe nne za  dunia

Uturuki yatoa fursa ya udhamini wa masomo

Abdullah Eren, kiongoni wa shirika la waturuki  na jamii ya waturuki waishio nje  ya Uturuki  apongeza hatua iliopigwa  na shirikisho hilo kwa kutoa udhamini wa masomo  kwa wanafunzi kutoka katika pembe nne za dunia.

Udhamini wa masomo kwa wanafunzi wa kimataifa umeanza tangu mwaka 2012.

Tangu mwaka 2012, Uturuki imekuwa ikitoa udhamini wa masomo kwa wanafunzi kutoka katika mataifa tofauti ulimwenguni.

Abdullah Eren akifanya mahojiano na  shirika la habari la Anadolu la Uturuki  amekumbusha kuwa siku ya mwisho ya kuomba adhamini wa masomo nchini Uturuki kwa mwaka 2019 ni Februari 20.

Shirikisho hilo ambalo linatambulika kama YTB linatoa udhamini wa masomo kwa wanafunzi  ambao wamemamliza shule ya upili wanataraji kuendelea na elimu ya juu.

Wanafunzi zaidi ya 42000 waliomba udhamini wa masomo mwaka 2012 na idadi hiyo kuongezeka mwaka 2018 ambapo watu 136 000 waliomba udhamini wa masomo Uturuki.

Lengo kuu la Makala haya  ni kuyatizama mashirika mbalimbali ya kujitolea ya kituruki ambayo yametekeleza na yanaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya aina tofauti duniani kote.

Wiki kadhaa zilizopita tuliangazia shirika la TIKA ( Wakala wa Uturuki uratibu wa maendeleo na ushirikiano  ). Kuanzia wiki hii tutaanza kuangazia shirika la YTB (Kurugenzi ya jamii za waturuki na ndugu zao waishio nje ya nchi). Shirika hili la kujitolea nalo limetekeleza miradi mbalimbali mikubwa maeneo tofauti.

Shirika la YTB lilianzishwa April 6 mwaka 2010. Lengo kuu la kuanzishwa shirika hili ni kuratibu shughuli za  kimasomo kwa waturuki na wanafunzi kutoka mataifa ndugu wa Uturuki wanaosoma nje ya Uturuki, lakini pia kuratibu shughuli za kimasomo kwa wanafunzi wa kimataifa wanaosoma nchini Uturuki.Kupitia kazi za shirika la YTB Uturuki imefanikiwa kuimarisha mahusiano na jamii ya waturuki waishio nje ya Uturuki lakini ia imefanikiwa kuimarisha mahusiano na mataifa rafiki ya Uturuki. Mahusiano hayo ni katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.

https://goo.gl/KaYZrY

 Habari Zinazohusiana