Supu ya dengu

Mapishi ya Kituruki

Supu ya dengu

Thamani ya supu katika vyakula vya kituruki ni tofauti sana. Kutoka zamani hadi sasa, ni moja ya vyakula vinavyopendwa sana  kati ya watu na taifa kwa ujumla. Supu katika tamaduni tofauti, kwa kawaida hunywewa jioni au katika chakula cha mchana,kwa waturuki supu hunywewa wakati wowote ule.

Kunywa supu kama kifungua kinywa asubuhi ni jambo la kawaida kati ya Waturuki. Katika vyakula vya kituruki, supu hutofautiana sana kutoka kwa vyakula vya aina nyingine kwa jinsi inavyotengenezwa .

Kwa mfano, katika jamii za magharibi, supu mara nyingi hu ana maji mengi na inakuwa nyepesi. Katika vyakula vya kituruki, kuna aina nyingi za supu, kuna supu nzipo na nyepesi,supu zenye nafaka na zile zisizo na nafaka na kuna supu ambazo hunywewa zikiwa baridi na nyingine hupendelewa zikiwa za moto.

Lakini supu ambayo ni tofauti kabisa na supu nyingine na hutengenezwa karibu katika kila nyumba,kila mgahawa na inaweza kuwa aina ya supu inayopendwa sana katika jamii ya waturuki ni supu ya dengu.

Leo tutatizama jinsi ya kutengeneza supu ya dengu yenye ladha halisia na rahisi sana kupika.

 

Mahitaji ni kama ifuatavyo:

 

1, 5 kikombe cha dengu

Kijiko 1 cha siagi (kijiko cha chakula)

Kijiko cha chakula 1 cha nyanya ya kusaga

 Kitunguu 1 kidogo kilichokatwa

1/2 kijiko cha pilipili nyekundu

1/2 kijiko cha pilipili manga

Kijiko 1 cha chumvi

Vikombe 6 vya supu ya nyama au maji

 

 

Tuanze kutengeneza supu yetu

 

 Osha dengu yako vizuri kabisa kwa maji mengi mpaka maji meupe yaishe. Kisha anza kupika vitunguu katika mafuta kwa dakika chache. Ongeza nyanya ya kusaga na uendeleee kukoroga kwa dakika chache zaidi. Ongeza dengu yak ona uendelee kukaanga.

.Baada ya dakika mbili, ongeza supu yako ya nyama au maji. Ongeza chumvi, pilipili manga na pilipili nyekundu, na hakikisha unapika kwenye moto wa kawaida kwa muda wa nusu saa.

Baada ya kuzima jiko lako chuja supu yak ona inakuwa tayari kwa kunywewa.

 

Furahia chakula chako!


Tagi: Uturuki , dengu , supu

Habari Zinazohusiana