Mauzo ya chai ya Uturuki yashamiri Uholanzi,Ufaransa na Ujerumani

Mauzo ya chai ya Uturuk katika mataifa ya nje yameshamiri kwa asilimia kubwa.

Mauzo ya chai ya Uturuki yashamiri Uholanzi,Ufaransa na Ujerumani

Mauzo ya chai ya Uturuk katika mataifa ya nje yameshamiri kwa asilimia kubwa.

Kwa sasa Uturuki inauza chai yake katika mataifa 42 tofauti,Ujerumani,Ufaransa na Uholanzi zikiwa katika mstari wa mbele katika orodha ya wanunuzi.

Kulingana na mkusanyiko wa data kutoka Chama cha Wasafirishaji wa bidhaa nchi za nje (NQF), faida ya dola 773,000 67 imepatikana ndani ya mwezi Januari kwa kuuza tani 318 za chai nchi za nje.

Hivyo, mauzo ya chai yameonekana kuongezeka kwa asilimia 110 ikilinganishwa na mwezi huo huo wa mwaka uliopita.

Ujerumani ipo katika nafasi ya kwanza kiwa imenunua chai yenye thamani ya dola  274,000 515,Ufaransa dola 165,000 232  na Uholanzi dola 85,000 .

Katika kipindi kama hicho cha mwaka uliopita, tani 151 za chai ziliuzwa kwa malipo ya dola 382,000 617.


Tagi: Uturuki , chai , mauzo

Habari Zinazohusiana