Mapishi ya Kituruki
Jinsi ya kutengeneza "sarma za nyama"

Watu wengi ulimwenguni hutengeneza chakula kwa kutumia majani na mboga. Wengine hutumia majani ya mahindi na ndizi, kama vile katika Amerika ya Kati na Amerika ya Kusini, au majani ya mitende au mianzi, kama ilivyo katika baadhi ya maeneo ya Mashariki ya Mbali. Uturuki hutumia karibu aina yote ya majani katika kutengeneza chakula. Waturuki hutumia bilinganya,artikke,nyanya,pilipili,maboga na hata kabeji. Tayari katika lugha nyingi, chakula hiki hujulikana kwa jina la "dolma au dolmades" kutoka katika kitenzi cha “dolmak” kwa waturuki wakimaanisha kujaza.
Leo tutawaonyesheni jinsi ya kutengeneza mjazo kwa kutumia majani ya mzabibu yani waturuki huita “sarma”.Chakula cha sarma kimetoka katika kitenzi cha sarmak ikimaanisha kufunika/kuzungushia. Kwa kawaida aina za namna hii za chakula kwa ujumla huitwa “Dolma” nchini Uturuki.Mjazo ukifanyika ndani ya majani ya mzabibu,kabeji au majani ya “chard” basi chakula hicho huitwa “Sarma”.
Mahitaji wakati wa kutengeneza sarma za nyama
Gramu 250 za majani ya mzabibu
Kitunguu 1 kilichokatwa katika vipande vidogo
250 gramu ya nyama iliyosagwa yenye mafuta kidogo
Kikombe 1 cha mchele
Vijiko viwili vya giligilani iliyokatwa vizuri
1/2 kijiko cha chumvi
1/4 kijiko cha pilipili manga
Kijiko 1 cha nyanya
Vijiko 3 vya mafuta
1.5 kikombe maji ya moto
1/2 kijiko cha chumvi
Jinsi ya kutengeneza “sarma za nyama”.
Kwanza, weka majani ya mzabibu katika maji ya moto kwa muda wa dakika 5 ili kuondoa chumvi.Toa majani yako katika maji ya moto na uyasuuze katika maji ya baridi kisha yaache yabaki bila maji.
Wakati huo huo,chukua bakuli uchanganye vitunguu,mchele uliooshwa na kukalishwa katika maji kwa muda kadhaa na nyama yako ya kusaga.Ongeza girigirani,pilipili na chumvi.Hakikisha unachanganya vizuri na mkono wako.Usitumie nguvu sana ili mchele usipondeke.
Chukua jani lako lililokauka na kisha litandaze na ukate mkia wake wa juu.Jaza mchanganyiko wako na uviringishe jani lako.
Fanya hivyo kwa majani yako yote.
Baada ya kujaza,panga majani yako katika sufuria kwa kuyababanisha katika mstari.Mstari wa kwanza ukijaa panga safu ya pili na kuendelea.
Mimina maji ya moto, mafuta ya mzaituni, nyanya na chumvi kwenye bakuli ndogo. Funika majani yako na sahani ya dongo ili yasiachane wakati wa kupika.
Pika katika moto mdogo kwa muda wa dakika arobaini.Sarma zako zipo tayari kwa kuliwa.Unaweza ukazila zikiwa zam oto au baridi na ukitaka unaweza kumwagia mtindi juu yake.
Furahia chakula chako!