Mturuki hunywa vikombe 1300 vya chai kwa mwaka

Mturuki hunywa vikombe 1,300 vya chai kila mwaka, kwa mujibu wa mkuu wa chama cha kahawa.

Mturuki hunywa vikombe 1300 vya chai kwa mwaka

Mturuki hunywa vikombe 1,300 vya chai kila mwaka, kwa mujibu wa mkuu wa chama cha kahawa.

Serdar Ersahin, mkuu wa chama hicho mjini  Istanbul amekiambia kituo cha habari cha Anadolu kwamba Uturuki ndiyo taifa la kwanza katika kunywa chai, kulingana na ripoti ya Kamati ya Kimataifa ya Chai.

''Waturuki hunywa vikombe 3-5 vya chai kila siku na idadi hiyo huongezeka hadi vikombe 10 wakati wa baridi'', Ersahin aliongeza.

Utamaduni wa kunywa chai ni muhimu kwa Waturuki kwani hutumia fursa hiyo kukutana na kufanya mazungumzo.

Chai nchini Uturuki hupikwa tofauti na nchi nyingine kwani unapaswa kuiweka katika moto kwa muda wa dakika 20.

Tagi: Uturuki , chai

Habari Zinazohusiana