Mauzo ya nyanya za Uturuki kushamiri nchini Urusi

Waziri wa kilimo na misitu wa uturuki Bekir Pakdemirli ametangaza kwamba Urusi imeridhia kiasi cha mauzo ya nyanya za Uturuki nchini humo kuongezwa mara mbili

Mauzo ya nyanya za Uturuki  kushamiri nchini Urusi

 

Waziri wa kilimo na misitu wa Uturuki Bekir Pakdemirli  ametangaza kwamba Urusi imeidhinisha kiasi cha nyanya inachonunua kutoka Uturuki. Kiasi hicho kimeongezwa kutoka tani 50 elfu mpaka tani laki moja.

Pakdemirli, aliyasema hayo akiwa nchini Ujerumani ambako alikwenda kuhudhuria mkutano wa 11 wa dunia wa kilimona chakula. Baada ya mkutano huo waziri huyo aliongea na wanahabari wa kituruki katika ofisi za ubalozi wa Uturuki. 

Pakdemirli alisema walikutana na waziri mwenzie kutoka Urusi na kubwa kabisa lililofanikiwa kwenye mazungumzo yao ni kuongeza kiasi cha mauzo ya nyanya Urusi kutoka tani 50 elfu mpaka tani laki moja.

 Habari Zinazohusiana