Shambulizi la Manbij limesababisha vifo vya watu 20 wakiwemo wanajeshi watano wa Marekani

Rais Erdoğan katika mkutano na waandishi wa habari akiwa na rais wa Kroatia amesema kwamba wanajeshi watano wa Marekani wamefariki katika  shambuli la Manbiji nchini Syria

Shambulizi la Manbij limesababisha vifo vya watu 20 wakiwemo wanajeshi watano wa Marekani

Rais Erdoğan katika mkutano na waandishi wa habari akiwa na rais wa Krotia amesema kwamba wanajeshi watano wa Marekani ni miongoni mwa watu waliofariki katika  shambuli la Manbiji nchini Syria

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan amesema kuwa anazo taarifa kuhusu  shambulizi la Manbij kuwa miongoni mwa watu 20 waliofariki katika shambulizi hilo wamo wanajeshi watano wa Marekani.

Hayo rais Erdoğan ameyazungumza katika mkutano na waandishi wa habari aliofanya na na rais wa Kroatia Kolinda Grabar Kitarovic ambae yupo katika ziara ya kikazi nchini Uturuki.

Kwa mujinu wa rais Erdoğan shambulizi hilo linawekuwa na lengo  la kushawishi  uamuzi wa Marekani kuondoa wanajeshş wake nchini Syria.

Rais Erdoğan amesema kuwa alielewa uamuzi wa Trump kuondoa wanajeshi wake Syria na kusema kwamba kitendo hicho cha kigaidi hakitoifanya Marekani kurudi nyuma  na knyume chake  itakuwa ni ushindi wa kundi la wanamgambo wa Daesh.

Amemalizi akisema kuwa  mapambano dhidi ya  Daesh yataendelea.Habari Zinazohusiana