Kaburi la Eyyubi Sultanı Süleyman Han lagunduliwa

Kaburi la Eyyubi Sultanı Süleyman Han, mtawala aliyeishi karne ya 14, lagunduliwa

Kaburi la Eyyubi Sultanı Süleyman Han lagunduliwa

 

Katika kazi inayoendelea ya kuhamisha kazi za kihistoria katika wilaya ya Hasankeyf jimboni Batman, kaburi la Eyyubi Sultanı Süleyman Han lagunduliwa.

Katika taarifa iliyotolewa na kiongozi wa Makumbusho ya Batman, Şeyhmus Genç inasema kwamba katika kazi  za uhamishaji wa kazi za kihistoria ikiwa ni pamoja na mnara wa msikiti uliojengwa mwaka 1407 na Sultan  Süleyman Han zinaendelea kwa kasi nzuri. na kwamba katika uchimbaji uliokuwa ukifanyika katika msikiti wa Süleyman Han walikutana na kaburi ambalo liliandikwa kuwa ni la Sultan Süleyman Han, wakati huo huo, kulikuwa na makaburi 6 mengine ambayo yalifikiriwa kuwa ya wanafamilia wa nasaba ya Ayyubid. Mifupa mawe na mchanga katika eneo hilo la makaburi ya Sultan Süleyman Han vilichukuliwa chini ya ulinzi na kisha kupelekwa Chuo Kikuu cha Mardin Artuklu kwa uchunguzi.


Tagi: Uturuki

Habari Zinazohusiana