Kazi za shirika la TİKA

Makala hii inaelezea kazi za shirika la TIKA

Kazi za shirika la TİKA

 

Katika makala hii wiki iliyopita tulielezea kwa ufupi kuhusiana na TİKA. Wiki hii pamoja na wiki inayofuata tutazungumzia kazi zinazofanywa na shirika la TİKA.

 

TİKA Inafanya Kazi gani ? Sehemu ya kwanza

TİKA ni kifupi cha maneno ya kituruki ambayo kwa kishwahili yanaweza kutafsiriwa kama Wakala wa Uturuki katika maendeleo na mahusiano ya kimataifa. Ni shirika lililoundwa katika msingi ya utamaduni wa kutoa misaada ,  kwa kuweza kufikisha misaada maeneo ya mbali kabisa ya dunia shirika hilo limeweza kuonyesha msimamo wa Uturuki katika kujali utu kwa vitendo.

Kutoka Mashariki ya kati hadi nchi za Balkani,  Kutoka Afrika hadi Amerika ya kusini na Asia ya kaskazini, Shirika la TİKA limeweza kutekeleza miradi mbambali ya kimaendeleo, kiuchumi,kijamii na kwenye maeneo mengine mengi . TİKA  inatumia rasilimali na uzoefu wa Uturuki kusaidia mataifa rafiki.

Mpaka hivi sasa miradi iliyotekelezwa na TİKA nje ya Uturuki inakaribia 25 elfu. Miradi hiyo inajumuisha ujenzi wa mahospitali, shule, barabara, pamoja na kuwasaidia maelfu ya wanyonge kukidhi mahitaji yao.

Kwa kazi zinazotekelezwa na TİKA  Uturuki imeweza kuimarisha mahusiano yake ya kirafiki na mataifa mbalimbali kufikia katika kiwango cha kuridhisha.

Miradi iliyotekelezwa ni ya nyanja mbalimbali kama vile Elimu,Afya, Makazi,Afya ya mama na mtoto, kilimo na ufaugaji, usafiri, uzalishaji, ajira, maji safi n.k. Malengo  makuu ya miradi yote hii ni kuyasaidia mataifa rafiki  kujenga uwezo wa kitaasisi na kibinadamu katika kutumia rasilimali zao kiufanisi . Katika malengo ya muda mrefu ni kujenga mahusiano na nchi hizo rafiki yaliyo katika misingi ya haki na usawa.

Katika miaka 3 iliyopita (2015-2017)  TİKA imefanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali ya kihistoria na kiutamaduni  ipatayo 250 . Miradi hiyo imetekelezwa maeneo tofauti kutoka Balkani mpaka Asia ya kati, kutoka Mashariki ya kati mpaka Afrika.

Hospitali zilizojengwa na TİKA katika nchi mbalimbali zikiwemo Somalia, Palestina, Sudan, Pakistan, Kırgızistan, Moldovia  na nyingine nyingi zimeendelea kutoa matibabu kwa maelfu ya watu kila siku.

                      


Tagi: TIKA

Habari Zinazohusiana