Erdoğan na uzalishaji wa bangi

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan, asema Uturuki itaanza kuzalisha bangi upya

Erdoğan na uzalishaji wa bangi

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan, amesema Uturuki itaanza tena kuzalisha bangi.

Erdoğan, alihudhuria kikao cha viongozi wa serikali za mitaa kilichofanyika ikulu na akufahamisha  kwamba maadui wa Uturuki ambao wanajifanya ni marafiki walichukua wazo la kuzalisha bangi Uturuki na sasa hivi wanauza bangi na kujipatia kipato.

Rais Erdoğan, alisema kwamba wizara ya kilimo imeshaanza mchakato kuhusiana na suala hilo la kilimo cha bangi na kwamba Uturuki itaanza kuzalisha bangi upya. 

Erdoğan, alisema katika miaka 16 ya uongozi wa chama cha haki na maendeleo (AK part) kiwango cha mfumko wa bei kimedumu katika wastani wa asilimia 9.54, kitu ambacho ni mafanikio makubwa  ukilinganisha na serikali zilizopita.

Rais Erdoğan, alisema kwamba Uturuki itaingia katika hatua ambayo litakuwa ni taifa lenye nguvu na lililoendelea na kwamba kuhusiana na jambo hilo mtu yeyeto asiwe na wasiwasi.Habari Zinazohusiana