Historia ya shirika la TİKA kwa ufupi

Historia ya shirika la TİKA kwa ufupi

Historia ya shirika la TİKA kwa ufupi

Kutoka katika kitengo cha Yunus Emre leo tutazungumzia kuhusu shirika la  Kızılay na TİKA,  mashirika ambayo yanahusika na misaada ya kiutu kştaifa na kimataifa katika sera  za nje na ndani za  Uturuki.

Mashirika haya yametafsiriwa kama mashirika ya   maendeleo ya kiuchumi.

Uturuki na mashirka hayo imesaini makubaliano na mataifa tofauti ya kikanda na mataifa mengine  kote ulimwenguni.

Leo katika kipindi chetu tutazungumzia kwa ufupi  historia ya  shirika la TİKA .

Shirika la TİKA limeundwa mwaka 1992 baada ya kumalizika kwa vita baridi . Shirika hilo liliundwa kwa niaba ya  kuanzisha na kuimarisha  ushirikiano na mataifa tofauti yenye uhusiano wa kihistoria na Uturuki.

undefinedfont-size:26px;">Baada ya kumalizika vita hivyo baridi  kuliundwa shirika hilo kuanza ushirikiano na URSS.

Miongoni mwa miradi ambayo ilianzishwa kati ya mwaka 1992 na mwaka 2002, ofisi takriban 12 zilifunguliwa  ambazo zilikuwa zikiwakilisha TİKA.

Miradi 2500 Na idadi ya mataifa yanayotaka kuendelea kushirikiana na Uturuki imezidi kuongezeka siku hadi siku.

Kwa sasa  TİKA ni shirika la kimataifa ambalo linapatikana katika mataifa 59 likiwa na ofisi 61 za uongozi na kuwa na malengo ya kufika katika mataifa 170.

Uturuki na washirika  wake ni kuwa na amani ya kudumu  kupitia shirika hilo eneo lolote lile ambapo  linapatikana.

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan  amesema kuwa  kote ulimwnguni  iwapo kutakuwa na watu wenye kuhitaji msaada basi shirika hilo na Uturuki haitosika kuwa pamoja nao.

Shirika la TİKA  linajitolea  katika maeneo tofauti ulimwwnguni katika miaka michache ya hivi karibuni.

Katika miradi yake , TİKA  inatoa msaada katika sekta ya afya, elimu na sekta nyingine a maendeleo.Habari Zinazohusiana