Uturuki yaadhimisha miaka 80 ya kifo cha baba wa taifa

Uturuki yaadhimisha miaka 80 ya kifo cha baba wa taifa Mustafa Kemal Atatürk

Uturuki yaadhimisha miaka 80 ya kifo cha baba wa taifa

Uturuki huadhimisha   kifo cha baba wa taifa Mustafa Kemal Atatürk kila ifikapo Novemba 10. Mwaka 2018 Uturuki imeadhimisha miaka 80 ya kifo cha baba wa taifa tangu kufariki kwake mwaka1938.

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan ameshiriki hafla hiyo ya maadhimisho ya  kifo cha baba wa taifa kwa kuweka shada la maua katika kaburi la Atatürk Anıtkabir mjini Ankara.

Rais Erdoğan ameongozana na mawaziri tofauti wakiwa wemo pia viongozi wa nagzi za juu katika jeshi la Uturuki.

Uturuki inaendelea kusonga mbele licha ya kushambuliwa mara kwa mara, Uturuki imeonesha   uwezo wake kwa kukutopoteza muelekeo na  kuendelea kuwa na matumaini  alendelea kusema rais Erdoğan.

Mustafa Kemal Atatürk alifariki Novemba 10  mwaka 1938 majira ya saa tatu na  dakika tano akiwa na umri wa miaka 57 baada ya kusumbuliwa na maradhi .Habari Zinazohusiana