Msimu mpya wa tamthilia pendwa ya “Diriliş Ertuğrul” wazinduliwa rasmi

Sehemu ya kwanza ya msimu mpya wa tamthilia “Diriliş Ertuğrul” imeanza kurushwa, na imerushwa katika nchi 80 katika lugha tofauti 25

Msimu mpya wa tamthilia pendwa ya “Diriliş Ertuğrul” wazinduliwa rasmi

Sehemu ya kwanza ya msimu mpya wa tamthilia “Diriliş Ertuğrul” imeanza kurushwa, na imerushwa katika nchi 80 katika lugha tofauti 25. Tamthilia hii ni tamthilia pendwa sana ambayo misimu iliyopita iliyovunja rekodi zote ya shirika la redio na televisheni la Uturuki, TRT.

Msimu huu mpya ni msimu wa tano, misimu iliyopita tamthilia hiiilivunja rekodi za TRT kwa kuangaliwa na watazaji wengi zaidi. Ni tamthilia ambayo inapendwa sana pia katika nchi nyingine.

Tamthilia hii imeimarishwa kwa kuongezwa waigizaji wapya. Tamasha lililo ambatana na chakula lilifanyi kakatika ukumbi wa Cemile Sultan Korusu jijini Istanbul ambapo waigizaji wote na mashabikiki waliangalia sehemu ya 122 ya tamthilia hio.

Katika tamasha hilo Mgurugenzi mkuu wa TRT İbrahim Eren naye alihudhuria, akizungumza katika tamasha hilo Eren alisema TRT inampango wa kuleta tamthilia zaidi zinazo akithi historia siku za usoni.

Tangu ianze kurushwa kwa mara ya kwanza mpaka sasa tamthilia hii imetizamwa mara bilioni 3.

 Habari Zinazohusiana