"TRT world" itaanza kupatikana moja kwa moja katika safari za ndege za, THY

Shirika la ndege la Uturuki THY limejumuisha katika katika kifurushi chake cha burudani chaneli ya TRT world ambayo inarusha matangazo ya moja kwa moja kwa lugha ya kiingereza

"TRT world" itaanza kupatikana moja kwa moja katika safari za ndege za, THY

Shirika la ndege la Uturuki ,THY limejumuisha katika ndege zake matangazo ya moja kwa moja kwalugha ya kiiingereza ya shirika la habari la televishen na radio la TRT.

Katika nchi 122 ambapo shirika hili ,THY linafanya safari zake sasa watakuwa na chagua lingine la chanzo cha habari za uhakika katika mtazamo mwingine.

Akiingolea habari hii  Mwenyekiti na mkurugenzi mkuu wa TRT Ibrahim Eren alisema ni muhimu kufahamu juu ya matukio yanayoendelea duniani na kupata habari kama jinsi zinavyotokea.

Wasafiri watapata fursa ya kupata habari za moja kwa moja za matukio muhimu kama yanavyotokea na sasa wameongezewa chanzo chengine cha habari chenye mtazamo wa kiaina yake alifahamisha Eren

"Kwa hili la THY kuwawezesha abiria wake kupata habari za matukio mbalimbali duniani katika mtazmo mpya wa aina yake kupitia TRT world tunashukuru sana" alisema Eren

TRT world ambayo makao yake makuu yako Istanbul ni jukwaa la habari za kimataifa na lilianza kurusha matangazo yake mwaka 2015, Linatoa mbadala wa chanzo cha habari kwa mtazamo mwingine kwa habari za kitaifa na kimataifa.

Shirika la ndege la Uturuki THY katika kifurushi chake cha burudani inatoa fursa ya kuangalia chaneli 8 za tv moja wapo ikiwa ni TRT world ambayo inarusha matangazo yake kwa njia ya satelaiti.


Tagi: TRT World , THY

Habari Zinazohusiana