Uturuki haina haja tena na IMF

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan asema kuwa Uturuki haina haja tena na Fuko la Fedha la Kimataifa

Uturuki haina haja tena na IMF

Rais wa Uturuki amesema kuwa viashirio vya kiuchumi nchini Uturuki vipo imara zaidi ya mataifa mengi ulimwenguni.

Hayo rais Erdoğan ameyazungumza katika  hotuba yake aliotoa katika mkutana wa 27 wa  chama cha AK mjini Ankara.

Hotuba hiyo imetolewa  wakati wa kutamatisha mkutano huo.

Katika hotuba hiyo rais Erdoğan amesema kuwa viashirio vya kiuchumi nchini Uturuki vipo imara na zaid ya mataifa mengi ulimwenguni.

Katika hotuba hiyo amesema kuwa  Uturuki imepiga hatua ambapo  haina haja ya  mkopo kutoka katika fuko la fedha la kimataifa.

Ukurasa wa Fuko la Fedha  la Kimataifa umekwishafunikwa amesema rais Erdoğan.

Baada ya mkutano huo rais Erdoğan amezungumza na waanshi wa habari kuhusu mwanahabari wa Washington Post Jamal Khashoggi ambae   hajulikani alipo  tangu Ijumaa baada ya  kujielekeza katika  ubalozi mdogo wa Saudi Arabia Uturuki.Habari Zinazohusiana