Mkutano wa kibiashara kati ya Uturuki na Afrika kufanyika Istanbul

Mkutano wa uchumi na biashara kati ya Uturuki na Afrika unatarajia kufanyika mjini Istanbul 10-11 Oktoba.

Mkutano wa kibiashara kati ya Uturuki na Afrika kufanyika Istanbul

Mkutano wa uchumi na biashara kati ya Uturuki na Afrika unatarajia kufanyika mjini Istanbul 10-11 Oktoba.

"Tunalenga kuboresha uhusiano wetu wa kiuchumi na kibiashara na nchi za Afrika na kuongeza uwekezaji kupitia jukwaa hilo," alisema waziri wa biashara wa Uturuki Ruhsar Pekcan.

Mkutano huo ni sehemu ya mpango wa hatua ya siku 100 ya serikali ya Uturuki ulionzishwa hivi karibuni kusaidia uchumi.

Pekcan aliongeza kuwa Uturuki imekuwa na hamu ya kufanya uwekezaji wa pamoja na nchi za Afrika.

Mkutano huo umeandaliwa na Bodi ya Uhusiano wa Uchumi wa Nje wa Uturuki (DEIK) katika uratibu na Wizara ya Biashara na Umoja wa Afrika.

Pekcan ameongeza kwa kusema kuwa Rais Recep Tayyip Erdoğan anatarajia kutoa hotuba ya ufunguzi kwenye jukwaa hilo. Rais wa Ethiopia Mulatu Teshome Wirtu pia anatarajiwa kuhudhuria mkutano huo.Habari Zinazohusiana