Uturuki yapongeza makubaliano ya amani kati ya Ethiopia na Eritrea

Uturuki kupitia wizara yake ya mambo ya nje imepongeza makubaliano ya amani yaliosainiwa kati ya Ethiopia na Eritrea

Ahmed Abiy.jpg
Türkiye dişişleri.jpg

 

Uturuki yapongeza makubaliano ya amani yaliosainiwa kati ya Eritrea na Ethiopia yaliosainiwa mjini Jeddah nchini Saudi Arabia.

Mkataba huo wa amani kati ya  Ethiopia na Saudi Arabia utaleta matumaini  na kudumisha amani katika mataifa hayo mawili ikiwemo pia eneo zima  la pembe la Afrika.

Makubalaino hayo yalikuwa yakisubiriwa kwa muda mrefu.

Katika taarifa iliotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Uturuki , Uturuki imepongeza makubaliano hayo. Makubaliano hayo yamesainiwa mjini Jeddah Septemba 16 akiwepo rais wa Eritrea Isaias  Afwerki na waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed.

Ushikiano kati ya Ethiopia na Eritrea ulivunjika tangu mwaka 1998. tangu Eritrea kujiondoa Ethiopia mwaka 1993.

Baada ya Eritrea kujitenga, mapigano yalizuka mwaka 1998 hadi mwaka 2000 ambapo inafahamishwa kuwa watu zaidi 70 000 walifariki.

 

 Habari Zinazohusiana