Waziri wa ulinzi wa Uturuki azungumzia usalama Idlib

Hulusi Akar, waziri wa ulinzi wa Uturuki azungumzia umuhimu wa kusitishwa mapigano Idlib Syria

Waziri wa ulinzi wa Uturuki azungumzia usalama Idlib

Waziri wa ulinzi wa Uturuki azungumzia umuhimu wa  kusitishwa mapigano Idlib nchini Syria.

Hulusi Akar amesema kuwa  iwapo kutaanzishwa  operesheni Idlib basi raia  na  hususan wanawake na watato ndio watakuwa waathirika katika operesheni hiyo.

Waziri wa ulinzi wa Uturuki alishiriki katika maadhimisho ya siku kuu ya uhuru ya Afghanistani mjini Ankara . Hafla ya maadhimisho ya uhuru  wa Afghanistan  imefanyika katika ofisi za ubalozi wake mjini Ankara.

Katika hafla hiyo waziri wa ulinzi wa Uturuki amezungumza na waandishi wa habari  kuhusu hali inayoendelea Idlib nchini Syria ambao amesema kuwa operesheni katika eneo hilo itakuwa na madhara makubwa kwa raia.

 

 Habari Zinazohusiana