Wahamiaji haramu 51 wakamatwa mkoani Van nchini Uturuki

Wahamiaji haramu 51 wakamatwa na jeshi la Polisi mkoani Van nchini Uturuki

Wahamiaji haramu 51 wakamatwa mkoani Van nchini Uturuki

 

Jeshi la Polisi mkoani Van limewakamata wahamiaji haramu 51 waliokuwa wakizurura karibu na mpaka wa Iran.

Jeshi la Polisi limewakamata  wahamiaji hao  likiwa katika wajibu wake wa kulinda usalama wa raia katika eneo hilo.

Wahamijai baada ya kufikishwa katika ofisi ya Polisi inayohusika na  wahamiaji haramu, wahamiaji hao wamebainika kuwa raia kutoka nchini Afghanistani na  Pakistani.

Wahamiaji hao wamepewa chakula  na maji naadae kupelekwa katika kituo cha afya cha Başkale kwa ajili  ya uchunguzi wa afya.

Mwanamke mmoja  mjamzito ni miomgoni mwa wahamiaji hao waliokamatwa na sasa anapewa matunzo katika hospitali moja Van.Habari Zinazohusiana