Rais wa Uturuki azungumzia kipato cha kundi la wahaini wa FETÖ Marekani

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan azungumzia kuhusu kipato cha kundi la wahaini wa FETÖ katika shule zake nchini Marekani

Rais wa Uturuki azungumzia kipato cha kundi la wahaini wa FETÖ Marekani

Rais wa Uturuki kwa mara nyingine amekemea  serikali ya Marekani kuhusu kundi la wahaini wa FETÖ.

Inafahamika vema kuwa kongozi wa kundi hilo anaishi nchini Marekani. Kundi la wahaini wa FETÖ amepewa hifadhi nchini Marekani.

Kundi la FETÖlinatuhumiwa na  serikali ya  Uturuki kuhusuka moja kwa moja na jaribio la mapinduzi la Julai 15 mwaka 2016 nchini Uturuki.

Rais Erdoğan amesema kuwa shule za kundi hilo zinazopatikana nchini Marekani  zinaingiza kipato cha  dola  milioni 850.

Hayo rais wa Uturuki ameyazungumza  Alkhamis jioni  katika mkutano na waandishi wa habari  akishirikiana na rais Benin katika ziara yake nchini Uturuki.

Rais wa Benin Patrice Talon  amefanya ziara nchini Uturuki.

Rais Erdoğan amezungumzia pia kuhusu umuhimu wa ushirikiano kati ya Uturuki na Benin na mataifa ya bara la Afrika kwa ujumla na kusema kwamba Uturuki imekwishafungua balozi  takribani 41  barani Afrika na inataraji kufungua balozi zake nyingine barani humo.

Suala la mapambano dhidi ya ugaidi limezungumziwa pia katika mkutano hu ona waandishi wa habari.  

Rais Erdoğan amezungumzia kundi la FETÖ ambalo amelifahamisha kuwa kundi hatari na kuipongeza Benin kwa ushirikiano wake.Habari Zinazohusiana