Urusi kuikabidhi Uturuki mfumo wa kujihami na makombora wa S-400 mwaka 2019

Mfumo wa kujihami na makombora wa S-400 kutoka Urusi kakabidhiwa Uturuki  mwaka 2019

Urusi kuikabidhi Uturuki mfumo wa kujihami na makombora  wa S-400 mwaka 2019

Mfumo wa kujihami na makombo wa S-400 ambao Uturuki imenunua kutoka Urusi unatarajiwa kukabidhiwa rasmi Uturuki ifikapo mwaka 2019.

Mfumo  huo una uwezo wa kuzuia makombora  ya masafa marefu ambayo  yatakuwa yamerushwa na maadui kwa lengo la kuishambulia Uturuki.

Uturuki imenunue  mfumo huo kwa ajili ya kujilindia usalama wake.

Kulingana na taarifa zilizotolewa na Interfax, shirika la ulinzi la Rosoboronexport  limefahmaisha kuwa  mfumo huo utakabidhiwa Uturuki katika kipindi cha miezi sita  ya mwanzo ya mwaka 2019.

Thamani ya mfumo huo inakadiriwa kuwa dola bilioni 2,5.

Uturuki itakauwa taifa la kwanza mwanachama wa NATO  kumiliki mfumo huo wa S-400.

 Habari Zinazohusiana