Rais Erdoğan : "Uturuki haiwezi kushindwa katika vita vya kiuchumi"

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan asema kuwa Uturuki haiwezi kushindwa katika vita vya kiuchumi

Rais Erdoğan : "Uturuki haiwezi kushindwa katika vita vya kiuchumi"

 

Rais wa Uturuki  amesema kuwa Uturuki  ipo katika vita vya kiuchumi na kamwe haiwezi kushindwa.

Akiwa katika ziara Bayburt, rais Erdoğan amezungumzia kuhusu  sarafu ya Uturuki  na kupanda kwa sarafu  ya kigeni kwa kusema kuwa Uturuki ipo katika vita vya kşuchumi na kamwe Uturuki haiwezi kushindwa.

Rais Erdoğan alizungumzia pia kuhusu suala hilo alipokuwa Rize.

Rais wa Uturuki amewataka raia kuwa wavumilivu na kuwakumbusha  kutazama nyuma  miaka 16 iliopita  Uturuki ilivyokuwa na ilikofikia  sasa. Rais Erdoğan ameendelea kusema kwamba  waturuki ni watu wanaochapa kazi  na kwa msaada wa muumba  Uturuki itashinda .

Amemalizia akisema kuwa kamwe Uturuki haitorudi nyuma katika malengo yake iliojiwekea ya mwaka 2023.

 


Tagi: Rize , uchumi , Erdoğan

Habari Zinazohusiana