Mabasi kutoka Uturuki kwa ajili ya uchukuzi yaanza kazi mjini Conakry

Mabasi kutoka nchini Uturuki kwa ajili ya shughuli za uchukuzi yaanza kazi mjini kati Conakry nchini Guinea

Mabasi kutoka Uturuki kwa ajili ya uchukuzi yaanza kazi  mjini Conakry

Mabasi kutoka nchini Uturuki  yaliokabidhiwa idara husika mjini Conakry yameanza kazi. Taarifa hiyo imetolewa na balozi wa Uturuki mjini Conakry.

Hatice Nur Sağman  , msimamizi wa  kidiplomasia wa Uturuki nchini Gunea ameliambia shirika la habari la Anadolu la Uturuki kuwa mabasi yaliokabidhiwa mamlaka husika kutoka nchini Uturuki  yamekwishaanza kazi mjini Kati Conakry.

Mabasi hayo yalianza kazi rasmi Agosti  Mosi.

Mabasi hayo 50 yalitolewa na rais wa Uturuki ecep Tayyıp Erdoğan  kwa rais aAlpha Conde  wakati wa ziara yake  nchini humo mwaka 2016.

Uongozi wa mabasi hayo umekabidhiwa  shirika moja la Uturuki kulingana na makubaliano na ofisi za meya wa jiji la Conakry.

Baada ya kumalizika uchunguzi wa kiufundi, muakilishi wa TİKA Ismail Gürlek amefahamisha kuwa ndipo mabasi hayo yaliruhusiwa kuanza kazi.

 Habari Zinazohusiana