Wahamiaji haramu 46 wakamatwa Magharibi mwa Uturuki

Wahamiaji haramu 46 wakamatwa katşka operesheni Magharibi mwa Uturuki

Wahamiaji  haramu 46 wakamatwa  Magharibi mwa Uturuki

Wahamiaji haramu 46 wakamatwa na jeshi la  kulinda mipaka katika kitongoji cha  Didim  mkoani Aydın nchini Uturuki.

Aydın ni mkoa unaoğpatikana Magharibi mwa Uturuki. Miongoni mwa watu waliokamatwa , wawili wamezuiliwa  wakishukiwa kuhusika na  uandalizi na   safari haramu za wahamiaji kuelekea nchini Ugiriki.

 Taarifa kuhusu kukamatwa kwa wahamiaji hao zimetolewa Jumatano na uongozi wa jeshi la Polisi Aydın.

Wahamiaji hao ni raia kutoka Syria ambao walikuwa na lengo la kujielekeza nchini Ugiriki kama atua yao ya kwanza ya safari zao kuelekea katika mataifa ya bara la Ulaya.

 

 Habari Zinazohusiana