Jeshi la Uturuki litaendelea kuimarisha usalama Kaskazini mwa Irak

Waziri wa ulinzi wa Uturuki asema kuwa jeshi la Uturuki litandelea kuimarisha usalama Kaskazini mwa Irak

Jeshi la Uturuki litaendelea kuimarisha usalama  Kaskazini mwa Irak

Waziri wa ulinzi wa Uturuki Nürettin Canikli asema kuwa  jeshi la Uturuki litandelea na operesheni zake Kaskazini mwa Irak hadi kutakapohakikishwa kuwa hakuna gaidi hata mmoja mpakani mwa Uturuki na Irak.

Waziri wa ulinzi wa Uturuki ameendelea kufahamisha kuwa  jeshi la Uturuki tangu kunza kwa mwaka 2018, magaidi zaidi ya 500 wamekwishaangamizwa Kaskazini mwa Irak.

Hayo waziri wa ulinzi wa Uturuki ameyazungumza akiwa muarifiwa  katika kituo cha habari cha Anadolu Jumanne mjini Ankara.

Akizungumzia kuhusu wanamgambo wa kundi la kşgaidi la PKK, waziri wa ulinzi wa Uturuki amesema kuwa  operesheni tofaut dhidi ya wanamgambo hao  zimeendeshwa na zitaendelea mkuendeshwa hadi kutakapohakikishwa kuwa hakuna gaidi hata mmoja katika eneo hilo.

 Habari Zinazohusiana