Rais wa Uturuki asema kwamba jeshi la Uturuki linaweza kuanza operesheni Sinjar wakati wowote

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan asema kuwa jeshi la Uturuki linaweza kuanza operesheni Sinjar wakati wowote ule

Rais wa Uturuki asema kwamba jeshi la Uturuki  linaweza kuanza operesheni Sinjar wakati wowote

Rais wa Uturuki katika mahojiano aliofanya katika kituo cha runinga amesema kuwa  jeshi la Uturuki linaweza kuanza operesheni yake Sinjar nchini Irak wakati wowote ule.

Jeshi la Uturuki limeshambulia ngome za wanamgambo wa kundi la kigaidi la PKK Kandil  nchini Irak. 

Rais Erdoğan amezungumzia  Sinjar na kusema kuwa Sinjar  haina utofauti wowote na Kandil.

Vile vile rais wa Uturuki amefahamisha kuwa Uturuki  itaendelea kuzungumza na Iran kuhusu  operesheni dhidi ya ugaidi.  Operesheni ilianzishwa Afrin nchini Syria dhidi ya  kundi la wanagambo wa PKK/PYD -YPG na kundi la wanamgambo wa Daesh imepelekea wanamgambo zaidi ya 4 600 kuangamizwa.

Rais Erdoğan amesema kuwa mapambano dhidi ya ugaidi yataendelea hadi kutakapo hakikishwa kuwa  hakuna gaiadi hata mmoja katika ardhi na mipaka ya Uturuki.

Rais wa Uturuki amezungumzia pia kuhusu   ahadi iliotolewa na Marekani kuwapokonya silaha magaidi Manbij  kama ilivyofahamishwa hapo awali.

Wakaazi wa Mnabij ni jamii ya waarabu kwa asilimia 90 hadi 95.  Baada ya magaidi wa PYD-YPG kuondoka Manbij  waarabu watarejea katika makaazi yao.

Katika mahojiano hayo rais Erdoğan ameendelea  akizungumzia suala zima la mfumo wa kujihami na makombora wa S-400 na kuibua mvutano kuhusu ndege za kivita za F-35.

Uturuki imetoa tayari kiwango cha  dola  milioni 800 kwa ajili ya ndege hizo na iwapo Marekani haitoheshimu makubaliano basi suala hilo litatatuliwa na vyambo vya sheria vya kimataifa.

 

 Habari Zinazohusiana