Mradi wa TANAP wazinduliwa nchini Uturuki

Mradi wa gesi wa "Trans Anatolian" (TANAP) umezinduliwa rasmi katika mji wa Eskişehir nchini Ututuki.

Mradi wa TANAP wazinduliwa nchini Uturuki

Mradi wa gesi wa "Trans Anatolian" (TANAP) umezinduliwa rasmi katika mji wa Eskişehir nchini Ututuki.

Mradi huo umezinduliwa na Rais Recep Tayyip Erdogan, Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev, Rais wa Ukraine Petro Poroshenko, Rais wa Serbia Aleksandar Vucic na Rais wa Jamhuri ya Kituruki ya Kaskazini ya Cyprus Mustafa Akinci,.

Akizungumza kwenye sherehe ya uzinduzi, Rais Erdogan ameuita mradi wa TANAP kuwa ni matunda ya nchi zinazohusika katika mradi huo na alisema kuwa utafungulia njia miradi mingine ya baadaye.

"Utulivu wa siasa na uchumi kwa miaka 16 iliyopita nchini Uturuki umechangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya mradi huo",alisema Erdoğan.

Rais wa Uturuki ameiuta mradi huo kama ishara mpya ya undugu kati ya Uturuki na Azerbaijan.Habari Zinazohusiana