Leo katika magazeti ya Uturuki

Leo katika magazeti ya Uturuki

Leo katika magazeti ya Uturuki

Sabah : « Rais Erdoğan atolea wito raia kuacha kubadilisha pesa walizonazo kwa sarafu za kigeni  »

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan awatolea wito raia kuacha kubalisha pesa walizonazo kwa sarafu za kigani. Rais Erdoğan ametoa wito huo akizungumzia  thamani ya sarafu ya kigeni Uturuki. « Nawatolea wito raia wa Uturuki  kuacha kubadilisha pesa zao kwa sarafu za kigeni ". Hayo rais wa Uturuki ameyazungumza Jumatano katika mlo wa iftar uliandaliwa ikulu. Rais wa Uturuki amewataka raia kuendelea kutumia sarafu ya Uturuki  kwa kusema kuwa ndşo uzalendo na iwaipo tutafanya hivyo basi tutakuwa tumeinusuru sarafu yetu na mabadiliko  mazuri tutayashuhudia. Kwa kumalizia , rais Erdoğana mesema kuwa  Uturuki imejikwamua katika mitihani iliojitokeza , kupanda kwa thamani ya sarafu ya kideni pia Uturuki itakabialana na jambo hilo kwa msaada wa muumba na raia.

Star : « Erdoğan : Hali ya sarafu ya kigeni  haiendani na uhalisia katika uchumi wa Uturuki »

Rais wa Uturuki amezungumzia hali ya kupanda kwa thamani ya sarafu ya kigeni kwa kusema kuwa hali hiyo haiendani na uhalisia na maendeleo yanayoshuhudiwa katika sekta ya uchumi wa Uturuki. Uturuki , uchumi wake umeongezeka kwa asilimia 7,4 mwaka uliopira na ni taifa ambalo ukuaji wake katika sekta ya uchumi inaridhisha. Uturuki imefikia  kiwango cha  dola bilioni 161 katika mauzo ya nje mwishoni mwa Aprili.  Kiwango hicho  kinatarajiwa kuongezeka na kufikia dola  bilioni 170 hadi ifikapo mwishoni mwa mwaka 2018.  Msimu wa kiangazi umewadia  na fursa kwa Uturuki kwa kuwa watalii zaidi ya  milioni 40 wanatarajiwa kutembelea nchini Uturuki na kuinua sekta ya uchumi. 

Vatan : «Uturuki yapiga atua katika sekta ya nishati »

Akşzungumza  katika mahojiano yaliofanyika katika kituo cha habari cha TRT , rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan  amezungumzia matukio tofauti  yanayozungumziwa katika vyombo vya habari  ikiwemo pia sekta ya nishati. Rais Erdoğan amesema kuwa visima vya mavuta  vitaanza kuchimbwa mkoani Hakkari. Kituo cha nyuklia cha Akkuyu Mersin ujenzi wake unaendelea na matokeo yake yatakuwa na faida kwa Uturuki na majirani zake katika sekta ya nishati.  Mradi wa TANAP  pia utapelekea usafirishaji wa gesi asilia  kutoka Azerbaijan kupitia Uturuki kuelekea Ulaya. Kituo kingine cha nishati ya jua ambacho kinauwezo wa kuzalisha megawatts 1000  mkoani Konya.

Yeni Safak : « Raia wa Iran  kuchagua Uturuki »Habari Zinazohusiana