Leo katika magazeti ya Uturuki

Leo katika magazeti ya Uturuki

Leo katika magazeti ya Uturuki

Sabah: « Rais Erdoğan aendelea na diplomasia kuhusu Palestina»

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan aendelea na diplomasia kuhusu  Palestina kwa ufanya mazungumzo na viongozi tofauti kama rais Urusi Vladimi r Putin, rais wa Iran Hassan Ruhani na Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel.  Viongozi hao katika mazungumzo yao na rais wa Uturuki wamezungumzia suala la Palestina na mauaji yalioendeshwa na jeshi la Israel Ukanda wa Gaza. Rais Erdoğan na Angela Merkel wamezungumzia mauaji ya Gaza na kusema kuwa ni kikwazo katika mazungumzo ya amani. 

Star: « Mzungumzo muhimu kati ya Uturuki na Marekani »

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlüt Çavuşoğlu  atafanya ziara nchini Marekani ifikapo Juni 4 ambapo atakutana na Mike Pompeo mjini Washington.  Wanadiplomasia hao watazungumzia suala zima la Syria,hali inayojiri Mashariki ya Kati, ushirikiano katika mapambano dhidi ya ugaidi na kundi la PKK na kundi la FETÖ/PYD.

Vatan: « Mazungumzo kati ya Hulusi Akar na Dunford »

Amiri jeshi mkuu wa Uturuki Hulusi Akar azungumza kwa njia ya simu na mwenziwe wa Marekani Joseph Dunford kuhusu ushirikiano katika sekta ya ulinzi na hali inayojiri  Mashariki ya Kati. Ripota wa shirika la habari la Anadolu amesekwa Hulusi Akar na amiri jeshi mkuu wa Marekani wamekutana baada ya mkutano wa NATO mjini Brussels.Viongozi hao ikiwa ni amiri jeshi mkuu wa Uturuki Hulusi Akar na amiri jeshi mkuu wa Marekani Joseph Dunford wamezungumzia  hali inajiri katika ukanda mzima wa Mashariki ikiwa pamoja na hali ya Ukanda wa Gaza na Syria.

Hürriyet: « Ujumbe wa waziri wa uchumi»

Waziri wa uchumi wa Uturuki Mehmet Şimşek  amepeprusha ujumbe kuhusu uchumi Uturuki katika ukurasa wake wa Twitter  akifahamisha kuwa Set ya kisiasa katika uchumi itajadiliwa baada ya uchaguzi na kuzidi kuimarishwa.

Yeni Şafak: «Misri na Israel zazuia mashirika ya Uturuki kutoa matibabu kwa majeruhi wa kipalestina »

Naibu waziri mkuu wa Uturuki Recep Akdağ  amesema kuwa Israel na Misri hazitoi ruhusa  kwa mashirika  ya Uturuki  yanayohusika na kuwasafirisha majeruhi Uturuki kwa lengo la kupewa matibabu kaada ya kujeruhiwa na jeshi la Israel katika  maandamano. Naibu waziri mkuu wa Uturuki akiwa katika ziara Cyprus Kaskazini amekemea mwenendo wa Israel  ambao ni wa kigaidi  ukiungwa mkono na Marekani  dhidi ya waislamu wa Palestina.Habari Zinazohusiana