Mtazamo

Uchaguzi wa mfumo wa urais nchini Uturuki. Kutoka Chuo Kikuu cha Ankara Yildirim Beyazit kitengo cha cha Sayansi za Siasa Dr. Kudret BÜLBÜL

Mtazamo

Mnamo Juni 24, 2018 Uturuki inatarajia kufanya uchaguzi wake mkuu wa 32 ikiwa ni uchaguzi wa kwanza kwenda katika mfumo wa urais.

Uchaguzi wa kwanza nchini Uturuki ulifanyika wakati wa utawala wa Ottoman mwaka 1876. Uchaguzi huu ulifuatiwa na uchaguzi wa 1878, 1908, 1912, 1914 na 1919. Chaguzi sita zilifanyika wakati huo.

Katika kipindi cha Republican, uchaguzi mkuu ulifanyika mara 25, ikiwa ni kipindi cha utawala wa chama kimoja. Katika kipindi cha utawala wa chama kimoja, uchaguzi wa 6 ulifanyika mwaka wa 1923, 27, 31, 35, 39, 43.Kuanzia mwaka wa 1946, wakati mfumo wa kisiasa wa vyama vingi ulipoanza, uchaguzi wa 19 ulifanyika wakati huo. Mnamo Juni 24, 2018, uchaguzi wa 20 utafanyika.

Kutoka Chuo Kikuu cha Ankara Yildirim  Beyazit kitengo cha Sayansi za Siasa Dr. Kudret BÜLBÜL anatufanyia tathmini ya mada yetu ya leo..

Uchaguzi wa kwanza ulifanyika nchini Uturuki mwaka 1876.Uchaguzi mkuu wa 24 Juni, 2018, utakuwa unafanyika baada ya miaka 142, ikiwa ni kwa mara 32. Kwa upande mwingine, kuna nyakati ambapo uchaguzi unashindwa kufanyika kama vile wakati wa jaribio la mapinduzi.

Nyakati tofauti za uchaguzi

Bila shaka kila uchaguzi, au kipindi cha uchaguzi, kina sifa zake. Uchaguzi uliofanywa katika kipindi cha Ottoman, kama vile Usultani  ni uchaguzi katika vipindi ya taasisi za kidini kama-Uislamu na Ukhalifa. Uturuki,katika kipindi cha usasa kuna utata kama Uislamu na Demokrasia vinapelekwa sambamba.

Uchaguzi kati ya 1923-1943 ni uchaguzi wa chama kimoja. Katika kipindi hiki,licha ya kuwa vyama vya upinzani havikuruhuiswa,utamaduni wa kufanya uchaguzş toka zama za Ottoman uliendelezwa.Jambo hilo lilikuwa la maana pia wakati wa Unazi NA Ufashisti pande za magharibi.Taratibu za uchaguzi ziliendelezwa.

Uturuki iliandika upya historia yake kwa kuanzisha mfumo wa vyama vingi mwaka 1946.Katika miaka ya 1876-1943 chaguzi zilifanywa katika ngazi mbili.Kutoka mwaka 1946 hadi sasa, uchaguzi umekuwa ukifanyika mara moja. Mfumo wa ngazi mbili ni sawa na mfumo wa Marekani wa leo. Katika mfumo huu, wapiga kura wanachagua wateule wao wa pili na wateule wa pili wanachagua manaibu wao. Mfumo wa ngazi mbili ni msingi wa ukosefu wa kujiamini kwa ujumla.

Juni 24, 2018 Uturuki,  kwa mara ya kwanza katika historia itafanya uchaguzi wa kuingia mfumo wa  urais na uchaguzi mkuu kwa wakati mmoja. Toka mwaka 1876 ​​mpaka leo serikali imekuwa ikichaguzliwa kivyake na bunge kivyake.Kwa mara ya kwanza bunge na serikali vitachaguliwa kwa pamoja. ”Kwa nini mfumo wa urasi ni muhimu kwa serikali ya Uturuki?”.Niliandika kuhusu suala hilo katika kitabu changu cha nguvu ya ”mfumo wa urais nchini Uturuki”.Kitabu hicho kiliandikwa kaba ya kura ya maoni mwaka 2017.

Maana ya uchaguzi

Demokrasia inachukua nguvu kutoka kwa uhalali wake, sio kutoka kwa njia iliyopo. Katika vipindi vya awali kulikuwa na njia tofauti za uhalali kwa mifumo ya kisiasa. Kunaweza pia kuwa na njia nyingine katika siku zijazo. Lakini katika dunia ya leo, demokrasia ni labda njia pekee ya kupata uhalali wa kijamii kwa mifumo ya kisiasa. Kwa hiyo, mfumo wa kisiasa kwa njia ya uchaguzi, huonekana kuwa na serikali ya halali ,huleta mshikamano na hivyo suala hilo ni muhimu. Mfumo wa kisiasa unaotumiwa na uchaguzi wa kitaifa kupitia uchaguzi una nguvu zaidi ndani ya nchi na vilevile kimataifa. Vinginevyo ni kweli kuwa mifumo ya kisiasa bila uhalali wa kijamii inapelekea serikali isio na shinikizo zaidi na hupelekea ukiukwaji wa haki za binadamu ambao ni hatari zaidi kwa sababu watu wao huchukua nguvu nje ya jamii zao. Kutokana na hili watu wanapaswa kutegemea watendaji zaidi wa kimataifa dhidi ya jamii yao wenyewe.

Tunapoangalia uhusiano kati ya demokrasia na maendeleo, ni rahisi kuona umuhimu wa uhalali wake katika jamii ikiwa ni sehemu ya mfumo wa kisiasa. Leo, nchi zilizoendelea zaidi na zenye mafanikio ni za kidemokrasia. Nchi za shida, na zenye matatizo ni zile zinazopingana na demokrasia. Katika mtazamo huu amani na utulivu sio chanzo cha maendeleo ya uchumi wa nchi bali maendeleo huletwa na demokrasi na vyama vingi.Hivi ndio vigezo vya maendeleo ya kiuchumi katika taifa. Ambapo hakuna amani hakuna maendeleo.

Demokrasia, uhuru, vyama vingi ni mfano halisi uliotekeleza sera ya maendeleo ya kiuchumi ya Uturuki baada ya miaka ya 2000. Kutokana na sera za kupinga demokrasia na jaribio la mapinduzi la Februari 28 kipato cha mwananchi kilishuka mpaka $ 2,000. Baada ya miaka ya 2000, maombi huria, demokrasia na uwingi wa sera vilipelekea kuongezeka kwa kipato mpaka $ 10,000.

Kwa kuzingatia kwamba Uturuki ilifanya uchaguzi wake wa kwanza mwaka 1876, ni nchi ambayo imekuwa na demokrasia tangu zamani. Japokuwa kumekuwa na serikali mbalimbali ndani ya miaka 142 , Uturuki imeendeleza jitihada zake katika demokrasia. Ukiangalia nyuma mazoea ya kupambana na demokrasia Ujerumani yani Nazism au Ufashista wa wataliano ,Uturuki haikuingia katika mfumo wa udikteta na badala yake imeonekana kudumisha demokrasia yake hasa baada ya miaka ya 2000.

Wapiga kura wa Kituruki hadi hii leo wameonyesha kuheshimu ahki zao za kidemokrasia  katika nchi kama Ujerumani, Austria na Uholanzi .Uturuki imekuwa ni mfano wa demokrasia kwa nchi nyingine

Uchaguzi nchini Uturuki ni uchaguzi wenye uzoefu wa miaka 142.Labda dunia inaweza kuutizama uchaguzi huu kwa jicho la karibu kutokana na kuwa uchaguzi wenye kuaminika

Kutoka Chuo Kikuu cha Ankara Yildirim Beyazit kitengo cha cha Sayansi za Siasa Dr. Kudret BÜLBÜL alipendekeza tathmini ya suala hilo.Habari Zinazohusiana