"Hakuna taifa lingine linalotoa matumaini kwa raia wa Syria kama Uturuki"

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan asema kuwa hakuna taifa lingine ambalo linatoa matumaini kwa rais wa Syria kama Uturuki

"Hakuna taifa lingine linalotoa matumaini kwa raia wa Syria kama Uturuki"

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan asema kuwa hakuna taifa lingine ambalo linatoa matumaini kwa raia wa Syria kama inavyofanya Uturuki.

Rais wa Uturuki  ameyasema hayo katika mkutano wa 6 wa chama tawala cha AK katika mkutano uliofanyika mjini Istanbul.

Rais Erdoğan katika hotuba aliotoa amesema kuwa  magaidi  wapatao 4 163 wameangamizwa  katika operrsheni ya Tawi la Mzaituni inayoendelea   Afrin. Operesheni hiyo ilianzishwa Januari 20 mwaka 2018 kwa lengo la kuwaondoa magaidi  wa kundi la PKK/PYD katika mipaka ya Uturuki na Syria.

Raia Erdoğan amefahamisha kuwa idara ya upelelezi ya Uturuki imefaulu kuwarejesha wafuasi 80 kwa kundi la FETÖ waliokuwa uhamishoni.

Rais Erdoğan amezungumzia pia mashambulizi yalioendeshwa na Marekani na washirika wake Syria . Mashambulizi hayo yalifahamishwa kuwa yalilenga vituo ambavyo vina silaha za kemikali , kwa mujibu wa rais Erdoğan mzozo wa Syria hautotatuliwa kwa muda mchache .

 Habari Zinazohusiana