Uturuki yatuma waraka Ujerumani baada ya miskiti kushambuliwa

Naibu waziri mkuu na msemaji wa serikali Bekir Bozdağ  amezungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano wa baraza la mawaziri kuhusu vitendo vya uhalifu dhidi ya miskiti Ujerumani

Uturuki yatuma waraka Ujerumani baada ya miskiti kushambuliwa

Bekir Bozdağ, naibu waziri mkuu na msemaji wa ikulu  amefahamisha kuwa Uturuki imetuma waraka nchini Ujerumani baada ya  miskiti  yenye kumilikiwa na waturuki kushambuliwa nchini Ujerumani.

Bekir Bozdağ baada ya mkutano wa baraza la mawaziri  alifahamisha kuwa Uturuki imetuma waraka huo Ujerumani unaohusu mashambulizi yaliolenga miskiti.

Akizungumzia kuhusu opereshyeni ya Tawi la Mzaituni ilioanzishwa kwa lengo la kuwaondoa magaidi mpakani mwa Uturuki na Syria, Bekir Bozdağ amesema kuwa jeshi la Uturuki limewaangamiza  magaidi zaidi ya 3300.

Amefahamisha kuwa wanajeshi 42 wa Uturuki wamefariki na wengine 202 ndio waliojeruhiwa tangu kuanza kwa operesheni hiyo.

Akizungumzia kuhusu operesheni Afrin , naibu waziri mkuu amesema kuwa katika siku chache za usoni magaidi wataondolewa moja kwa moja katika eneo hilo.

Kwa mara nyinginr Bekir Bozdağ amefahamisha kwa msisitizo kuwa raia wanalindwa vilivyo katika operesheni ya Tawi la Mzaituni.

Akizungumzia mashambulizi yanayolenga nyumba za ibada nchini Ujerumani, msema wa serikali  amekekemea wafuasi wa makundi ya kigaidi nchini Ujerumani ndio wanaoshambulia miskiti.Habari Zinazohusiana