Uturuki ina mpango wa kuvutia watalii wengi mwaka huu

Waziri wa utalii wa Uturuki Numan Kurtulmuş amesema kuwa nchi yake ina mpango wa kuvutia watalii wengi zaidi 2018.

Uturuki ina mpango wa kuvutia watalii wengi mwaka huu

Waziri wa utalii wa Uturuki Numan Kurtulmuş amesema kuwa nchi yake ina mpango wa kuvutia watalii wengi zaidi 2018.

Kwa mujibu wa habari,waziri huyo amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa idadi ya watalii kuvunja rekodi mwaka huu.

Aidha waziri Numan ametathmini idadi ya watalii mwaka 2016-2017 na kusema kuwa watalii waliongezeka kwa kasi mwaka 2017 ukilinganisha na 2016.

Ripoti zinaonyesha kuwa takriban watalii milioni 32.4 waliitembelea Uturuki 2017.

Ni jumla ya dola bilioni 26 zimepatikana kutokana na utalii nchini humo.

Uturuki ina matumaini ya kufikisha watalii milioni 38 mwaka 2018.Habari Zinazohusiana