Waziri wa Ujerumani atembelea shule ya wakimbizi wa Syria mjini Ankara

Waziri wa serekali wa Ujerumani, Maria Böhmer, aliitembelea shule moja mjini Anakara wanaposoma wanafunzi wakimbizi kutoka Syria.

Waziri wa Ujerumani atembelea shule ya wakimbizi wa Syria mjini Ankara

Waziri wa serekali wa Ujerumani, Maria Böhmer, aliitembelea shule moja mjini Anakara wanaposoma wanafunzi wakimbizi kutoka Syria.

Böhmer alijielekeza jumatatu katika shule hiyo inayotowa mafunzo ya ufundi ambao ilijengwa kwa udhamini wa shirika la Marafiki wa Syria.

Wanafunzi wa shule hiyo inayojulikana kama Mashujaa wa Demokrasia wa Julai 15, hupata mafunzo ya ufundi kama kuchoma vyoma, ujenzi, fundi cherehani, kubuni tovuti, na kadhalika.

Baada ya kuingia kila darasa, Maria Böhmer alionyesha umuhimu wanawake kujiunga na shule hiyo wakiwa wengi.

Maria Böhmer amekumbusha kuwa Ujerumani inafadhili mashule ya ufundi kwa wasyria, na huwa inafadhili miradi tofauti ya kusaidia wakimbizi wa Syria nchini Uturuki kwa kiwango cha Euro milioni 150 kila mwaka.

 Habari Zinazohusiana