Uturuki kupokea kwa mikono miwili wanaochangia kufikia malengo yake ya 2023

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, amesema kuwa wanafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha Uturuki inashinadana na nchi nyingine kwenye nyanja zote hasa teknolojia.

Rais Erdoğan alichapisha ujumbe kwenye akaunti yake ya Tweeter Jumatano, akikumbusha kuwa kufikia malengo ya 2023, taasisi na watu binafsi wanapaswa kuendeleza utamaduni wa kubuni na kuendena daima na teknolojia ya kisasa.

Rais Erdoğan aliandika kuwa milango ya Uturuki yiko wazi kwa wale wote wanaoweza kutoa mchango kwa Uturuki, na miradi katika sekta ya teknolojia ya anga, na magari itaendelea sambamba kwa ushirikiano wa wale walio tayari kuungana na Uturuki. Kwa msaada wake Mungu, na kazi za wananchi, Uturuki itafika  kwenye ustaarabu wa kisasa unaoifaa.

Habari Zinazohusiana