Aamir Khan asema filamu yake mpya inahusu wanawake

Nyota wa Bollywood Aamir Khan amesema kuwa filamu yake mpya Secret Superstar ni hatua katika kuleta usawa kati ya wanawake na wanaume.

Aamir Khan asema filamu yake mpya inahusu wanawake

Nyota wa Bollywood Aamir Khan amesema kuwa filamu yake mpya Secret Superstar ni hatua katika kuleta usawa kati ya wanawake na wanaume.

Muigizaji huyo mwenye umri wa miaka 52 aliwasili Istanbul siku ya Jumatano kwa ajili ya kuitangaza filamu yake baada ya kualikwa na waziri wa utamaduni wa Uturuki.

Kwa mujibu wa habari,filamu hiyo inayohusu wanawake sana itazinduliwa rasmi mnamo 20 Oktoba mwaka huu.

Aidha Aamir Khan amesema kuwa wanawake wamekuwa wakisahaulika sana na sasa ni wakati wa kuleta uelewa wa usawa wa kijinsia.

Filamu ya Secret  Superstar inahusu msichana mwenye umri wa miaka 14,anavyohangaika kutimiza ndoto yake ya kuwa mwanamuziki.

Muigizaji huyo vilevile amesema kuwa haijalishi kama ni mwanamke au mwanaume,lazima kuwe na haki sawa kwa wote dunaini.Habari Zinazohusiana