Nyota wa Bollywood Aamir Khan apokewa na mamia Istanbul

Nyota wa filamu za kihindi Aamir Khan amepokelewa na umati wa watu katika mkutano wake wa kuitangaza filamu yake mpya Istanbul

Nyota wa Bollywood Aamir Khan apokewa na mamia Istanbul

Nyota wa filamu za kihindi Aamir Khan amepokelewa na umati wa watu jijini Istanbul.

Nyota huyo katika mkutano na waandishi wa habari istanbul amesema kuwa amefurahishwa kujua kwamba wananchi wengi Uturuki hufuatilia na hupenda filamu zake.

Kwa mujibu wa habari,Aamir Khan amewasili Uturuki kwa nia ya kutangaza filamu yake mpya ''Secret Superstar''.

Aamir Khan wakati akizungumza amesema kuwa yeye kama muigizaji hajawahi kuelewa ni kwanini mashabiki wanampenda muigizaji mmoja kuzidi mwingine au ni vipi muigizaji mmoja akapata umaarufu zaidi kuliko wengine bali yeye kama yeye anaichukua kazi ya uigizaji kama kazi anayoipenda kutoka moyoni.Na wakati akiigiza hujisikia amani na furaha sana.

Filamu ya ''Secret Superstar'' inatarajia kurushwa katika sinema 20 Oktoba.Habari Zinazohusiana