Jaribio la mapinduzi laambukia patupu Uturuki

Juhudi za jaribio la mapinduzi ya kijeshi zaambulia patupu nchini Uturuki

Jaribio la mapinduzi laambukia patupu Uturuki

Kundi moja la baadhi ya wanajeshi wa Uturuki linaloshukiwa kuwa wafuasi wa FETO lilithubutu kutekeleza jaribio la mapinudzi ya kijeshi katika mji wa Ankara na Istanbul nchini hapo jana usiku.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alitoa maelezo baada ya tukio hilo na kusisitiza kuwa wahusika wa jaribio hilo wataadhibiwa kisheria.

Akizungumza kwenye televisheni moja, rais Erdogan alitoa wito wa mshikamano kwa wananchi na kuwahimiza kukusanyika kwenye sehemu za umma ili awasilishe ujumbe huo.

Erdogan pia aliwaomba wananchi kuwa na utulivu na kusisitiza kuwa yeye ndiye amiri mkuu wa majeshi yote kwa mujibu wa katiba na kwamba hakuna harakati zozote za mapinduzi zitakazoweza kufanikiwa dhidi ya serikali.

Waziri mkuu wa Uturuki Binali Yıldırım naye aliahidi kutoa adhabu kali kwa wahusika wa jaribio la mapinduzi baada ya kukamatwa na kuwasilishwa kwa vituo vya polisi.

Kwa upande mwengine shirika la habari la kitaifa la TRT lilivamiwa kwa kufungwa kwa muda lakini baadaye hali ikarudi kuwa ya kawaida na matangazo yakaanza kupeperushwa.

Spika wa bunge kuu la kitaifa TBMM Ismail Kahraman aliita mkutano wa dharura bungeni huku viongozi wa vyama vya upinzani Kemal Kılıcdaroglu na Devlet Bahceli wakionyesha msimamo wao wa kupinda vikali mapinduzi.Habari Zinazohusiana