Bei ya viza ya Schengen kupanda

Bei ya viza ya Schengen kupanda kutoka Euro 60 mpaka Euro 80

Bei ya viza ya Schengen kupanda

 

Kamati ya Bunge la Umoja wa Ulaya imepitisha pendekezo la kupandisha bei ya viza ya Schengen kutoka Euro 60 hadi Euro 80.

Ongezeko hilo halitawahusu ndugu wa raia wa nchi za Umoja huo, wanafunzi, watafiti na watoto chini ya miaka 12. Wasanii, wanamichezo na wengine wote wanaosafiri mara kwa mara watapatiwa viza inayowaruhusu kuingia na kutoka mara nyingia kwenye eneo hilo la Schengen.

Kuanzia miezi 9 kabla ya safari unaweza kuomba viza kwa mujibu wa utaratibu mpya.

Ili pendekezo hilo liwe sheria na kuanza kutumika inabidi lipigiwe kura na mkutano mkuu wa umoja huo .

Eneo la Schengen linaundwa na nchi 26, na raia zaidi wa nchi 60 wanaruhusa ya kusafiri eneo la Schengen bila kuhitaji viza. Rais wa nchi 100 wanahitaji viza kuingia katika eneo la Schengen.

 

 Habari Zinazohusiana