Bombadier kupunguza maelfu ya wafanyakazi

Shirika la utenegenezaji wa ndege la Bombardier kupunguza maelfu ya wafanyakazi katika kuboresha ufanisi

Bombadier kupunguza maelfu ya wafanyakazi

Shirika la ujenzi wa ndege,usafirishaji na teknolojia la nchini Kanada,Bombardier, limefikia uamuzi wa kupunguza wafanyakazi elfu 5.

Katika tangazo lilitolewa na shirika hilo linasema ndani ya miezi 12 hadi 18 ijayo watapunguza wafanyakazi elfu 5.

 Pia tangazo hilo lilisema kuwa shirika hilo limefikia uamuzi wa  kuuza chapa yao ya ndege " Q series" kwa thamani ya dola milioni 900 na chapa yao ya "Havilland" kwa thamani ya dola milioni 300.

Akizunguzia mpango wa kuliunda upya shirika hilo kiongozi wa ngazi za juu wa Bombardier,Alain Bellamare alisema wameanzakuchukua hatua za kulifanya shirika hilolifikie uwezo wake wa juu kabisa wa mafanikio.

Ukiangalia mapato ya shirika hilo katika robo ya tatu ya mwaka huu kabla ya kodi ukilinganisha na ya mwaka uliopita kwa kipindi hiko yameongezeka kwa kiasi cha dola milioni 267.

Shirika hilo limejipangia kwa mwaka 2019 kuongeza mapato yake kwa asilimia 10, hivyo kufikia dola bilioni 18.

Bombardier limeajiri wafanyakazi 69,500 dunia nzima.

 Habari Zinazohusiana