Tume kutoka Uturuki yafanya mazungumzo  na Iran kuhusu ushirikiano katika biashara

Tume kutoka katika shirika la wafanyabiashara  wa Uturuki MÜSİAD  yafanya mazungumza na Iran kuhusu ushirikiano katika  biashara

Tume kutoka Uturuki yafanya mazungumzo  na Iran kuhusu ushirikiano katika biashara

Tume kutoka katika shirika la wafanyabiashara wa Uturuki MÜSİAD  yafanya mazungumza na Iran  kuhusu ushirikiano katika sekta ya biashara kati ya  Uturuki na Iran.

Mkutano katika  wajumbe wa tume hiyo na viongozi husika katika sekta ya biashara wa Iran  umefanyika  makao makuu ya  chumba cha  ushirikiano cha Iran mjini Tehran.

Katika mkutano wao viongozi hao wamejadili  kuhusu mbinu ambazo zitapelekea  kuimarisha ushirikiano katika biashara bain aya Uturuki na Iran.

Viongozi walioshiriki katika mkutano huo ni pamoja na  mshauri wa kibiashara  katika ubalozi wa Uturuki mjini Tehran, Cengiz Gürsel, mkurugenzi wa Müsiad tawi la Trabzon Ali Kaan  na  mkurugenzi wa chumba cha biashara cha Iran Mohamed Ali Zighami wakiwemo pia wafanyabiashara wakubwa kutoka Uturuki.

Gürsel amesema kuwa kiwango  katika ushirikiano wa kibiashara kati ya Uturuki na Iran ni kidogo mno ikilinganishwa na ukaribu na mpaka uliopo kati ya mataifa hayo mawili.

Uturuki na Iran ni mataifa ambayo yana ukaribu  wa kitamaduni.

Kiwango cha ushirikiano kati ya Uturuki na Iran  mwaka 2017 katika sekta ya biashara kilifikia dola bilioni 10.Habari Zinazohusiana