Uturuki yapendekeza mataifa ya D-8 kutumia sarafu za kitaifa katika biashara

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlüt Çavuşoğlu ametoa pendekezo katika kikao cha D-8 kutumia sarafu za kitaifa katika biashara

Uturuki yapendekeza mataifa ya D-8 kutumia sarafu za kitaifa katika biashara

Uturuki yatoa pendekezo la kutumia sarafu za kitaifa katika  sekta ya biashara  kati ya mataifa wanachama wa D-8.

Mevlüt Çavuşoğlu, ametoa pendekezo hilo katika ufunguzi wa mkutano wa mawaziri wa  D-8.

 Çavuşoğlu, amesema ili kuweza kwenda sambamba na mabadiliko ya kiuchumi yanayotokea duniani D-8 inabidi ishirikiane na Uturuki katika kuyakabili matatizo hayo.

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki pia alisema,  tuunaishi katika zama ambazo bei za kubadilisha fedha za kigeni zinatumika na baadhi ya mataifa kwa sababu  za kisiasa.

Ulimwengu upo katika zama za vita za kibiashara. Suluhisho la suala hili ni kutumia pesa za mataifa yetu tunapofanya bishara .

Çavuşoğlu amesema kwamba Uturuki, Uchina, Urusi na Ukrain zinajiandaa kuanza kutumia sarafu  zao za kitaifa katika biashara  na mazungumzo na mataifa mengine juu ya suala hili yanaendelea.

Suala hilo pia linaweza kufanyika miongoni mwa mataifa ya D-8, hivyo Mevlüt akapendeza kwa mataifa hayo waanzishe kitengo maalum cha uthaminishaji wa fedha za mataifa hayo "Clearing House".

 Habari Zinazohusiana