Makubaliano kati ya Uturuki na Umoja wa Afrika kuandaa  jukwaa la ushirikiano

Uturuki na Umoja wa Afrika zasaini  makubaliano  kundaa jukwaa  la ushirikiano kwa pamoja

Makubaliano kati ya Uturuki na Umoja wa Afrika kuandaa  jukwaa la ushirikiano

Jukwa na biashara la pamoja kati ya Uturuki na Umoja wa Afrika   katika biashara lina lengo la  kuwaweka pamoja  viongozi wa mashirika na makampuni ya Afrika na Uturuki.

Uturuki na  Umoja wa Afrika  wameafikiana   Jumatatu  ushirikiano na kuandaliwa mkutano wa pili wa kibiashara  ambao unatarajiwa kufanyika ifikapo  Oktoba  mjini Istanbul.

Balozi wa Uturuki nchini Ethiopia Fatih Ulusoy amesaini  makubaliano hayo  akimuakilisha waziri wa  biashara  wa Uturuki huku Umoja wa Afrika  ukiwakilishwa na Harrison Victor.

Saini hiyo ya makubaliano  imesainiwa mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Ulusoy amesema kuwa  Uturuki ina lengo la kuwa na ushirikiano ulio na nguvu  na mataifa ya bara la Afrika na kuendelea kufahamisha kuwa  matumaini katika mkutano  huo wa pili  ni  kufikia  makubaliano  ya ushirikiano katika biashara.Habari Zinazohusiana