Rais wa Sudani Omar al Bashir ateua baraza jipya la mawaziri
Rais wa Sudani Omar al Bashir amevunja na kuteua baraza jipya la mawaziri kwa lengo la kukabiliana na mzozo wa kiuchumi

Rais wa Sudani Omar al Bashir amevunja baraza mawaziri na kuunda baraza jipya ikifahamishwa kuwa ni kwa lengo la kukabiliana na mzozo wa kiuchumi nchini humo.
Uamuzi huo wa rais wa Sudani umechukuliwa hapo Jumapili ambapo pia waziri mkuu mpya ameteuliwa.
Motazz Musa ndie ameteuliwa katika wadhifa wa waziri mkuu nchini Sudani.
Rais wa Sudani aliitisha mkutano wa dharura na kufahamisha kwamba baraza jipya la mawaziri linahitajika kwa lengo la kutatua mgogoro uliopo katika sekta ya uchumi.