Uturuki kuanza kuchimba  mafuta na gesi asilia Mediterania

Uturuki yataraji kuanza kuchimba mafuta na gesi asilia  katika bahari ya Mediterania  hivi karibuni

Uturuki kuanza kuchimba  mafuta na gesi asilia Mediterania

Uturuki inatarajia kaunza kuchimba mafuta na gesi asilia katika bahari ya Mediterania katika siku hivi karibuni.

Uchimbaji huo  wa mafuta unatarajiwa kuendeshwa  katika eneo la  Mediterania Mashariki.

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlüt Çavuşoğlu asema kuwa Uturuki katika muda mfupi ujao itaanza  kuchimba mafuta katika eneo la Mashariki mwa Bahari ya Mediterania.

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki akishirikiana na waziri wa  mambo ya nje wa Jamhuri ya Kituruki ya Cyprus Magharibi Kudret Özersay wamefanya mkutano na waandishi wa habari .

Mkutano huo na  waandishi wa habari kati ya viongozi hao umefanyika mjini Ankara katika ziara yake  nchini Uturuki.

Mkutano huo ulifanyika katika ofisi za wizara ya mambo ya nje mjini Ankara.

Akihojiwa kuhusu  harakati za uchimbaji wa mafuta katika bahari ya Mediterania, waziri wa  mambo ya nje wa Uturuki amejibu kuwa  katika kulinda  mazingira na maji safi, Uturuki itaendelea  kuchukua maamuzi ambayo  yanakwenda sambamba  na hatua muhimu na Jamhuri ya Cyprus Kaskazini  itashirikishwa.

Mevlüt Çavuşoğlu amekumbusha kuwa Uturuki ilizuia  baadhi ya  hatua za uchimbaji wa mafuta katika Bahari ya  Mediterania. Ameendelea pia kuzungumzia kuhusu uchimbaji huo na kufahamisha kuwa waziri wa fedha wa Uturuki Berat Albayrak  anafuatilia suala hilo .Habari Zinazohusiana