Uturuki kuishtaki Marekani katika shirika la kimataifa la biashara WTO

Uturuki kuishtaki Marekani katika Shirika la kimataifa la biashara baada ya kuwekewa vikwazo katika bidhaa zake za chuma

Uturuki kuishtaki Marekani katika shirika la kimataifa la biashara WTO

Uturuki kuishtaki Marekani katika shirika la kimataifa la biashara WTO  baada ya Marekani kuchukuwa uamuzi wa  kuongeza  kodi katika bidhaa za chuma kutoka Uturuki.

WTO ni shirika la kimataifa la biashara ambalo linahusika na uratibu wa  biashara kimataifa.

Uturuki kupitia wizara yake ya biashara imefahamisha  Jumatatu kuwa Uturuki kwa ushirikiano na mataifa kama India, China, Uswisi, Norway, Canada, Urusi, Mexico na Umoja wa Ulaya itaishtaki Marekani katika shirika la kimataifa la biashara.

Tangazo lililotolewa na wizara hiyo limesema kuwa Uturuki itaendelea kuwalinda  wafanyabiashara wake  kwa kuheshimu  haki  za wafanyabiashara.

 Habari Zinazohusiana