Makala ya CNN kuhusu hali ya uchumi nchini Uturuki

CNN imeandika makala ikielezea hali ya uchumi nchini Uturuki.

Makala ya CNN kuhusu hali ya uchumi nchini Uturuki

CNN imeandika makala ikielezea hali ya uchumi nchini Uturuki.

Shirika la habari la kimataifa la Marekani CNN,limeandika makala likielezea jinsi nchi za maghari zitakavyopata hasara kubwa kuipoteza Uturuki kama mshirika katika sekta ya uchumi.

Hii ni baada ya Marekani kuanzisha vita vya kiuchumi na Uturuki siku chache zilizopita.

Makala hiyo imeandikwa kwa lengo la kuzionya nchi za magharibi kuhusu hali ya uchumi ya sasa nchini Uturuki.

"Nchi za magharibi hazipo tayari kuipoteza Uturuki",kilisema kichwa cha habari cha makala hiyo.

Utafiti umeonyesha kuwa hali ya kiuchumi inayoendela kwa sasa nchini Uturuki itaathiri kwa kiasi kikubwa nchi za magharibi.

Katika makala hiyo imeelezewa pia kuwa ni vyema kwa Uturuki kupokelewa katika Umoja wa Ulaya haraka iwezekanavyo ili kuliokoa jahazi.

 

 


Tagi: uchumi , Uturuki , makala , CNN

Habari Zinazohusiana