"Uchumi wa Uturuki waendelea kuimarika licha ya mashambulizi kutoka huku na kule"

Rais wa Uturuki apongeza sekta ya uchumi nchini Uturuki licha ya mashambulizi kutoka pande zote kwa lengo la kuudhoofisha

"Uchumi wa Uturuki waendelea kuimarika licha ya mashambulizi kutoka huku na kule"

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan apongeza sekta ya uchumi  ya Uturuki kwa kuimarika kwake licha ya kushambuliwa pande zote kwa lengo la kutaka kuudhoofisha.

Uchumi wa Uturuki umeimarika katika  kipindi cha muda mfupi ikilinganishwa na mataifa mengine ulimwenguni.

Hayo rais Erdoğan ameyazungumza Jumatatu. Rais wa Uturuki  amesema kuwa uchumi  umeimarika kwa asilimia 7,4 katika kipindi cha  mitatu ya mwanzo ya mwaka 2018.

Uturuki inashika nafasi ya 2 katika mataifa ya G20.

Ujumbe kuhusu kuimarika kwa uchumi wa Uturuki rais Erdoğan amemtoa katika ukurasa wake wa Twitter.

Licha ya mashambulizi ambayo yanalenga  kudhoofisha uchumi wa Uturuki, sekta ya uchumi ya Uturuki imesimama kidete  kukabiliana na mashambulizi hayo.

 Habari Zinazohusiana