Rais Erdoğan aahidi mabadiliko katika sekta ya uchumi Uturuki

Rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan aahidi mabadiliko katika sekta ya uchumi iwapo atachaguliwa kwa mara nyingine Juni 24

Rais Erdoğan aahidi mabadiliko katika sekta ya uchumi Uturuki

Rais wa Uturuki Recep  Tayyıp Ertdoğan  katika mahojiano aliofanya katika runinga ya Bloomberg  amesema kuwa atafanya mabadiliko makubwa katika sekta ya uchumi  iwapo atachaguliwa kwa mara nyingine  katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Uturuki ifikapo Juni 24.

Rais Erdoğan amesema kwamba mfumo wa fedha Uturuki  utakuwa sawiya na mfumo wa kimataifa na kulifanya taifa la Uturuli kuwa imara katika sekta yake ya uchumi.

Katika mahojiano hayo kuhusu uchumi na mabadilikom yanaotarajiwa rais Erdoğan amesema kuwa  hatua thabiti zitachukuliwa  ili kuhakikisha kuwa maslahi ya Uturuki yanalindwa. Rais Erdoğan amesisitiza kuwa maslahi ya Uturuki yatapewa kipaumbele.

 Habari Zinazohusiana